East African Journal of Swahili Studies, Volume 5, Issue 1, 2022 Article DOI: https://doi.org/10.37284/eajss.5.1.527 12 | This work is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License. East African Journal of Swahili Studies eajss.eanso.org Volume 5, Issue 1, 2022 Print ISSN: 2707-3467 | Online ISSN: 2707-3475 Title DOI: https://doi.org/10.37284/2707-3475 EAST AFRICAN NATURE & SCIENCE ORGANIZATION Original Article Athari za Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi Katika Fonolojia Arudhi. Cheruiyot Evans Kiplimo & Dkt. Leonard Chacha Mwita, PhD 1 1 Chuo Kikuu cha Kenyatta, S.L.P 43844 00100, Nairobi, Kenya. * ORCID ID: https://orcid.org/0000-0002-0526-7068; Barua pepe ya mawasiliano: cheruiyotevanskiplimo@gmail.com DOI ya Nakala: https://doi.org/10.37284/eajss.5.1.527 Tarehe ya Uchapishaji: 13 Januari 2022 Istilahi Muhimu: Fonolojia Arudhi, Kusambaa Kwa Shadda, Likwidi, Shadda, Silabi Na Udondoshaji Wa Kihistoria. IKISIRI Kiswahili ni lugha mojawapo ya Kiafrika inayochangia ujifunzaji wa fonolojia. Wanaisimu wamejadili mifanyiko ya kifonolojia katika Kiswahili bila kugusia swala la athari zake katika vipashio vikubwa kuliko fonimu. Hata hivyo, siyo mifanyiko yote ya kifonolojia ndio huathiri fonolojia arudhi ya lugha husika. Fonimu zinapoungana ili kuunda vipashio vikubwa vya lugha kama vile silabi na neno, zinaathiriana katika viwango mbalimbali. Athari zingine huwa ndogo kiasi kwamba hazionekani bayana ilhali athari zingine huwa kubwa kiasi cha kuonekana bayana. Mfanyiko wa kifonolojia unaohusishwa na utowekaji wa fonimu ni udondoshaji. Fonimu inapotoweka katika neno, vipashio vikubwa kuliko fonimu yenyewe hupokea athari katika mfumo wa lugha. Makala hii inaonyesha jinsi mabadiliko ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi huathiri fonolojia arudhi ya Kiswahili. Hili liliwezekana kwa kujenga umbo la awali la neno kisha kuonyesha jinsi kudondoshwa kwa fonimu kuliathiri fonolojia arudhi. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya fonolojia zalishi iliyoasisiwa na Chomsky na Halle (1968). Makala hii, imetegemea data ya maktabani iliyokusanywa kwa kusoma, kudondoa na kunakili. APA CITATION Kiplimo, C. E. & L. C. Mwita. (2022). Athari za Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi Katika Fonolojia Arudhi. East African Journal of Swahili Studies, 5(1), 12-24. https://doi.org/10.37284/eajss.5.1.527 CHICAGO CITATION Kiplimo, Cheruiyot Evans & Leonard Chacha Mwita. 2022. “Athari za Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi Katika Fonolojia Arudhi”. East African Journal of Swahili Studies 5 (1), 12-24. https://doi.org/10.37284/eajss.5.1.527. HARVARD CITATION Kiplimo, C. E. & L. C. Mwita (2022) “Athari za Udondoshaji wa Kihistoria wa Fonimu za Likwidi Katika Fonolojia Arudhi”, East African Journal of Swahili Studies, 5(1), pp. 12-24. doi: 10.37284/eajss.5.1.527.