MAANA, SIFA NA MAJUKUMU YA USHAIRI Ni utungo wa kisanii wenye mpangilio maalum wa lugha ya mkato katika usemi na uimbaji na wenye mpangilio maalimu katika uwasilishaji. Dhana ya ushairi hairejelei mashairi pekee bali pia huhusisha nyimbo na tenzi. Shairi ni utungo wa kisanaa wenye lugha ya mkato, lugha hii hutumia taswira kwa wingi. Wimbo ni utungo ulio na maneno yanayosomeka kimziki. Assumpta Matei katika Fani ya Fasihi Simulizi, uk. 92 anasema kuwa nyimbo ni tungo za kishairi zenye mahadhi na kushuka kwa sauti, muwala na mapigo ya kimuziki na huwasilishwa kwa kuimbwa. Tenzi ni tungo za kishairi zinazosimulia historian a sifa za vitu au watu. Tenzi huwa na kipande kimoja na beti nyingi. Lugha katika mashairi huwa ya mkato na yenye mvuto wa aina yake. Lugha hii huathiri na kugusa msomaji. Aidha, hutumia maneno machache yanayopangwa ipasavyo ili yaimbike au yakaririke. Sifa za Tungo za Kishairi 1. Maneno huwa ya lugha ya mkato. Isiyo wazi. 2. Kuna beti na mishororo 3. Tungo hizi huweza kukaririwa au kuimbwa. 4. Ala za mziki zaweza kutumika. 5. Maudhui yapo. 6. Taswira na jazanda hutumika kwa wingi. USHAIRI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI 23 Items Created by DERICKCHARLESLUGAYE Powered by